In Summary

•Bradley Mtall amepokea viatu vya kushonwa kutoka kwa kampuni ya Bata kwa mara ya pili wiki moja baada ya kupokea jozi ya kwanza

•Bata inasema kiatu cha Bradley kimekuwa kikubwa zaidi kuwahi kutengenezwa na kampuni hiyo.

Bradley Mtall
Image: Bradley Mtall Genz Goliath//Facebook

Bradley Mtall amepokea jozi lingine la viatu vya kushonwa kutoka kampuni ya Bata.

Kijana huyo anayetambulika kama Gen Z Goliath amepokea viatu vingine vya kufungwa wiki moja tu baada ya kupokea jozi ya kwanza.

Katika chapisho la video na picha, Bradley alionekana akiwa katika kampuni ya Bata akivaa viatu ambavyo alikuwa ameshonewa.

Aliandika kuwa ni kampuni moja pekee ambayo inaweza kuvisha miguu yake kubwa viatu.

"Kunapokuwa na miguu mikubwa ya kuvisha kiatu, kuna kampuni moja tu inayoweza kufanya hivyo. Bata Kenya wanajivunia kumzawadi  Bradley viatu vyake vya kwanza vilivyofungwa," aliandika.

Katika taarifa, kampuni ya Bata ilisema kuwa imeweka historia kwa kutengeneza kiatu kubwa zaidi. Viatu hivo ambavyo vina ukubwa wa 58 UK ndivyo viatu kubwa zaidi Bata imewai kutengeneza.

"Bata Kenya imeweka historia kwa kukabidhi rasmi saizi kubwa zaidi ya kiatu kuwahi kuzalishwa na kampuni...Kiatu cha ukubwa wa saizi 58 UK ndivyo viatu kubwa zaidi kuwahi tengenezwa na Bata," Bata.

Wiki iliyopita kijana huyo alipata viatu vilivyofungwa kwa mara ya kwanza maishani mwake kutoka Bata baada ya kukaa muda mrefu bila kuvaa viatu.

“Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa kampuni ya kutengeneza viatu ya Bata kwa fursa hii ya kubadilisha maisha yangu kabisa,fursa ya kuvaa viatu vilivyofungwa kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Hii ina maana kubwa zaidi kwamba ambayo hata ninakosa maneno ya kuelezea, na kwa kweli ninashukuru sana jitihada zenu. Ninatazamia kufanya kazi zaidi na nyinyi kwenye miradi mingi na yenye maana siku zijazo,” Bradley aliandika.

View Comments