In Summary

• Aliambatanisha picha ya pamoja wakiwa na Samidoh na kumuomba radhi kwa chochote ambacho huenda alifanya na kikamkwaza msanii huyo.

SAMIDOH NA MARITE.
Image: FACEBOOK

Aliyekuwa meneja wa msanii Samidoh, Moses Marite amevunja kimya chake siku chache baada ya msanii huyo kutangaza kusitisha uhusiano wao wa kikazi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Marite aliandika ujumbe mrefu akimshukuru Samidoh kwa kumpa nafasi ya kufanya kazi naye kama mratibu wa shughuli zake za muziki.

Aliambatanisha picha ya pamoja wakiwa na Samidoh na kumuomba radhi kwa chochote ambacho huenda alifanya na kikamkwaza msanii huyo.

“Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Samidoh, HSC kwa kuniamini na kunipa nami nafasi ya kuwa sehemu ya bendi yake kubwa. Kila nafasi ya kutumikia ni zawadi; asante kwa kuniruhusu nifanye na wewe,”

“Msaada wako umekuwa mkubwa sana. Kupitia wewe, nimefanikiwa mengi ambayo yanaweza kuhusishwa na wewe tu. Pole zangu za dhati kwako kwa matukio ambayo nimekukosea wewe na chapa yako kwa kujua na bila kujua nilipokuwa nikitekeleza majukumu yangu,” Marite balisema.

Akiangazia nyuma safari ambayo wakutembea na Samidoh, Marite alisema kwamba anaondoka katika majukumu yake kama meneja akiwa ameinua shingo juu kwa madaha mno kutokana na kazi nzuri ambayo aliifanikisha kwa chapa ya Samidoh kimuziki.

“Walakini, imekuwa safari iliyojaa viwango vya juu na vya chini sawa. Siwezi kuwashukuru zaidi mashabiki wetu wapendwa na wafuasi kwa kusimama nasi kupitia na kupitia. Nimepata marafiki wakubwa katika safari hii,” alisema.

Siku chache zilizopita, Samidoh alichapisha kupitia Instagram akiwatahadharisha mashabiki na wateja dhidi ya kushiriki biashara yoyote na Marite kwa niaba yake, kwani alikuwa amemtema kama meneja wake.

“Chukua tahadhari kubwa kwamba Samidoh Entertainment ilisitisha huduma zote za Moses Marite ambaye picha yake inaonekana. Chukua tahadhari zaidi kwamba hana uwezo wa kufanya biashara yoyote kwa niaba ya Samidoh,” ujumbe huo ulisoma.

View Comments