logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanawake wawili waliokuwa wakihadaa watu kuwa mawakili wakamatwa Kasarani

Wanawake wawili waliokuwa wakijifanya kuwa wakili wamekamatwa mjini Kasarani.

image
na Davis Ojiambo

Habari29 February 2024 - 11:44

Muhtasari


  • Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kujifanya na kughushi nyaraka za kisheria.

Polisi siku ya Jumatano, waliwakamata wanawake wawili wanaoshukiwa kuendesha ofisi wakihadaa wananchi kuwa ni mawakili katika eneo la  Kasarani, Nairobi.

Wawili hao walikamatwa na maafisa wa upelelezi na maafisa wa Chama cha Wanasheria nchini (LSK) walipokuwa wakiendesha shughuli zao kutoka katika orofa moja karibu na kituo cha polisi cha Kasarani.

Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kujifanya na kughushi nyaraka za kisheria.

Timu ya LSK  inayoongozwa na Stephen Mbugua ilisema mawakili bandia sasa wamebadilisha mbinu zao na kuamua kufanya kazi katika maeneo ya makazi.

"Nyaraka mbalimbali za miamala zilipatikana kutoka kwa wawili hao, ikiwa ni pamoja na uhamisho wa mali na wosia," Mbugua alisema.

Aliwaonya wananchi na wanataaluma wenzake wa taaluma ya sheria dhidi ya kuwaandikisha watu wasio na sifa za kufanya kazi za kisheria akisema wana hatari ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufutiwa usajili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved