In Summary

•Umoja wa Mataifa unasema wakimbizi milioni moja sasa wameikimbia Ukraine na kuelekea nchi jirani.

Image: REUTERS

Watu milioni moja wameikimbia Ukraine , UN imesema

Umoja wa Mataifa unasema wakimbizi milioni moja sasa wameikimbia Ukraine na kuelekea nchi jirani.

Hatua hiyo imefanyika ndani ya siku saba pekee. Uvamizi wa Urusi ulianza Alhamisi iliyopita.

Kama mwandishi wa BBC Lewis Goodall anavyaelezea: "Mgogoro wa wakimbizi wa 2015 ulihusisha wakimbizi milioni 1.3. Hiyo inakaribia kuipiku idadi ya wanaotoka Ukraine katika wiki moja."

Katika taarifa yake kwenye Twitter, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi Filippo Grandi aliomba "kusitishwa kwa vita , ili msaada wa kibinadamu uweze kutolewa" kwa mamilioni ya raia waliosalia nchini humo.

Shirika hilo limetabiri mzozo huo utawaacha takriban watu milioni 12 wakiwa wakimbizi wa ndani na kuhitaji msaada.

Ramani hii inaelezea zaidi kule ambako raia wa Ukrain wanatorokea.

View Comments