In Summary

•Vikosi vya serikali vilishambulia kambi za Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji mkuu Khartoum, na Bahri kaskazini mwake.

Image: BBC

Jeshi la Sudan limefanya mashambulizi makubwa dhidi ya kundi lenye nguvu la kijeshi linalopigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, likilenga maeneo ya mji mkuu iliyopoteza mwanzoni mwa mzozo huo.

Katika mashambulizi ya alfajiri siku ya Alhamisi, vikosi vya serikali vilishambulia kambi za Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika mji mkuu Khartoum, na Bahri kaskazini mwake.

Sudan imetumbukia katika vita tangu jeshi na RSF lilipoanza mapambano makali ya kuwania madaraka mwezi Aprili 2023, na kusababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa umekiita mojawapo ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Takribani watu 150,000 wameuawa katika mzozo huo huku zaidi ya watu milioni 10, karibu theluthi moja ya watu, wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

Mashahidi waliripoti mashambulizi makali ya angani na mapigano makali siku ya Alhamisi wakati wanajeshi walipovuka madaraja mawili muhimu juu ya Mto Nile, ambayo yalikuwa yametenganisha maeneo yanayodhibitiwa na serikali huko Omdurman na mikoa inayodhibitiwa na RSF.

Tangu mwanzoni mwa vita, wanamgambo wamekuwa wakidhibiti karibu mji mkuu wote.

View Comments