In Summary

• Mwanaume huyo aliripotiwa kumchukua mama yake kwenda kutafuta chakula cha mifugo shambani na kumbaka.

• Mwanamke huyo alisema katika maelezo yake kuwa mwanawe alimpeleka shambani, akamziba mdomo, kumbaka na kumshinikiza kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

Mshukiwa akiwa ametiwa pingu ndani ya seli.
Image: HISANI

Mwanamume mwenye umri wa miaka 38 amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mama yake mwenye umri wa miaka 60 huko Uttar Pradesh's Bulandshahr nchini India, runinga ya NDTV imeripoti.

Mwanaume huyo alimbaka mama yake Januari 16 mwaka jana, ambapo kaka yake aliripoti kwa polisi.

Mahakama ya haraka ilimpata na hatia na kutoa uamuzi wake siku ya Jumatatu.

"Kesi hii ya ubakaji ilisajiliwa takriban mwaka mmoja na nusu nyuma, mwanamke alimtuhumu mwanawe kwa ubakaji, polisi walikuwa wamesajili," mkuu wa polisi alisema.

Wakili wa serikali Vijay Kumar Sharma alisema hajawahi kukutana na kesi kama hii katika taaluma yake. “Mama huyo aliendelea kulia na kurudia kusema, ‘Mwanangu alinibaka’.

Mwanaume huyo aliripotiwa kumchukua mama yake kwenda kutafuta chakula cha mifugo shambani na kumbaka.

Mwanamke huyo alisema katika maelezo yake kuwa mwanawe alimpeleka shambani, akamziba mdomo, kumbaka na kumshinikiza kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara.

“Nilikunja mikono na kumbembeleza lakini alinibaka, nikawa najisemea kikongwe, nikapoteza fahamu, nilipozipata alinitishia kuniua endapo nitamueleza mtu tukio hilo, akaniuliza pia kulala naye kila usiku,” mama mkongwe alieleza mahakama.

Mume wa mwanamke alikufa miaka 10 nyuma.

Daktari aliyemchunguza mwanamke huyo alisema kuwa mwili wake haukuwa na dalili ya kuumia nje au ndani.

Ikinukuu hukumu ya awali, mahakama ilibainisha kuwa hata daktari aliyemchunguza mwathiriwa hatapata dalili za ubakaji, si sababu ya kutoamini ushahidi wa mlalamishi.

View Comments