In Summary

• ODPP imepata ushindi wa washukiwa wa ufisadi walioshtakiwa mahakamani kupatikana na kesi ya kujibu.

• Saba hao wanashtakiwa kwa kuwa na njama ya kufanya uhalifu wa kiuchumi kinyume na kifungu cha 47A (3)  cha sheria ya kupambana na rushwa na uhalifu wa kiuchumi ya mwaka 2003.

Mahakama ya Milimani jijini Nairobi

Mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi ya Milimani imewapata washukiwa 7 wa ufisadi na kesi ya kujibu iliyowasilishwa na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma (ODPP) kortini humo.

Mahakama hiyo mnamo Alhamisi 26, iliwapata wafanyakazi 7 wakuu wa kampuni ya kusambaza nguvu za umeme nchini KPLC na kesi ya kujibu inayohusisha uhalifu wa kiuchumi wa shilingi milioni 150.

Saba hao watatakiwa kudhibitishia mahakama kuwa hawana hatia katika kesi wanaohusishwa nayo kutoka kwa ODPP.

Katika kesi iliyowasilishwa na ODPP, washukiwa wanashtakiwa kwa kuwa na njama ya kufanya uhalifu wa kiuchumi kinyume na kifungu cha 47A (3)  cha sheria ya kupambana na rushwa na uhalifu wa kiuchumi ya mwaka 2003.

Vile vile wana mashtaka ya tuhuma ya kushindwa kwa makusudi kutii  sheria ya kifungo sawia cha sheria ya mwaka 2003.

Saba hao ni ikiwemo wanachama 4 wa kamati ya kutathmini kandarasi kwa majina Noah Ogano Omondi, John Mwaura Njehia, James Muriuki na Benard Muturi.

Wengine ni meneja mkuu wa fedha Harun Karisa, mkuu wa ugavi Daniel Ochieng Muga na mwanacha katika kamati ya ufunguzi wa zabuni Evelyne Pauline Amondi.

Washukiwa hao vile vile wanakabiliwa na shtaka la utumizi mbaya wa afisi kinyume na kifungu  cha 46 kilichosomwa kwa pamoja na kifungu cha 48 (1) cha vita  dhidi ya rushwa na uhalifu wa kiuchumi vya mwaka 2004.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa washukiwa walitumia njia za ujanja katika mchakato wa kutoa kandarasi ambapo wazabuni walihitimu bila vigezo vinavyostahili.

Pia, walikiuka sheria kwa kufanya malipo ya shilingi milioni 150 yasiyo ya kawaida kwa wakandarasi.

Mahakama itatoa maelezo zaidi kuhusu saba hao tarehe 15, Oktoba  wakati washukiwa watatakiwa kuelezea namna watajitetea mahakamani.

View Comments