In Summary

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Trans Nzoia, Homa Bay, Migori, Murang'a, Meru, Kiambu, na Kilifi.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Septemba 26. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Trans Nzoia, Homa Bay, Migori, Murang'a, Meru, Kiambu, na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi , sehemu za mtaa wa Mwihoko zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kachibora na Kaplamai Centre katika kaunti ya Trans Nzoia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Homabay na Asumbi katika kaunti ya Homabay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Awendo na Ranen katika kaunti ya Migori pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Murang'a, maeneo ya Punda Milia na Makuyu Girls yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Akaiga na Kunati katika kaunti ya Meru yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya KVM, Chania Feeds, Capwell, mji wa Ruaka na Kigwaru-Inn katika kaunti ya Kiambu yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Mnarani na Mavueni katika kaunti ya Kilifi pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

View Comments