Covid 19
5 zaidi wafariki huku 551 wakipatikana na Corona
Nairobi inaongoza kwa visa 212 ,kilifi ina visa 39 ilhali Mombasa ina visa 35.
- Idadi ya watu waliofariki kwa ajili ya virusi hivyo imeongezeka hadi 1,474 baada ya watu 5 kuaga dunia .
- Wagonjwa Wengine 266 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 55,610 idadi ya waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa.
Kenya leo imesajili visa vipya 551 vya corona baada ya sampuli 4,675 kupimwa na kufikisha jumla ya visa hivyo kufika 84,169 ,amesema katibu wa utawala wa wizara ya Afya Rashid Aman
Idadi ya watu waliofariki kwa ajili ya virusi hivyo imeongezeka hadi 1,474 baada ya watu 5 kuaga dunia .
Aman amesema kuna wagonjwa 1,275 katika hospitali mbali mbali nchini huku wengine 8,070 wakiwa chini ya utunzi wa nyumbani . wagonjwa 71 wapo katika kitengo cha ICU huku 18 wakiwa katika kitengo cha HDU
Wagonjwa Wengine 266 wamepona ugonjwa huo na kufikisha 55,610 idadi ya waliopona ugonjwa huo hadi kufikia sasa.
Kutoka visa hivyo vipya 525 ni wakenya ilhali 26 ni raia wa kigeni .wagonjwa 301 ni wanaume huku wanawake wakiwa 250 .Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa siku saba ilhali wa umri wa juu ana miaka 100 .
Nairobi inaongoza kwa visa 212 ,kilifi ina visa 39 ilhali Mombasa ina visa 35.