In Summary

• Serikali ya Urusi sasa imetangaza kiwango kipya cha pesa ambacho Mtu anaweza kutuma nje ya taifa hilo.

• Kwa raia wa Urusi kuanzia sasa hawatoruhusiwa kutuma nje ya Nchi zaidi ya dola 10000 na wasio wananchi wa Urusi  hawatoruhusiwa kutuma nje ya Nchi, dola 5000 .

 

KWA HISANI
Image: Dola ya kimarekani

Katika jitihada za kupambana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi yake na Mataifa mbalimbali, Serikali ya Urusi sasa imetangaza kiwango kipya cha pesa ambacho Mtu anaweza kutuma nje ya taifa hilo.

Kwa raia wa Urusi kuanzia sasa hawatoruhusiwa kutuma nje ya Nchi zaidi ya dola 10000 na wasio wananchi wa Urusi  hawatoruhusiwa kutuma nje ya Nchi, dola 5000 .

Hali hii inatarajiwa kuibua kipindi kigumu kwa wafanyiashara wa Urusi ambao wamewekeza katika mataifa ya nje na sasa watalazimika kutafuta mbinu mbadala ili kuhakikisha mambo yao yanaendelea vizuri.

Hatua hii inalenga kuzuia mataifa mbalimbali kufaidi kutokana na uchumi wa Urusi kipindi hiki wanazidi kusukuma vita vya kijeshi dhidi ya taifa la Ukraine.

Ifahamike kwamba siku chache zilizopita, kampuni mbalimbali zilisitisha huduma zao nchini Urusi kwa kile walichokitaja kama kutokuwepo kwa mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

 

View Comments