Watu wengi wanatatizika kwa sababu ya kukosa huduma bora za afya. Baadhi yao ambao wanaugua wamekosa tumaini.
Mamlaka ya Afya ya Jamii, Social Health Authority, yaani SHA, iko hapa kuleta mabadiliko.
SHA ilibuniwa ili kurahisisha na kupunguzia Wananchi mzigo wa gharama za matibabu.
Mtu yeyote anayeishi nchini Kenya anafaa kujisajili upya na Social Health Authority hata kama alikuwa amesajiliwa na NHIF.
Jisajili kwa kubonyeza *147# au kupitia www.sha.go.ke.
Wananchi pia wanaweza kujisajili kwenye kituo cha afya cha serikali kilicho karibu nao,au tawi la SHA au katika vituo vya Huduma Centre.