In Summary

• Uwanja wa Kirigiti unakaribia kukamilika baada ya ujenzi uliong'oa nanga mwaka wa 2020.

• Waziri wa michezo Kipchumba Murkomen amedokeza kuwa jina litabadilishwa pindi ujenzi unakamilika na baada ya kuhusisha umma.

Uwanja wa Kirigiti
Image: Hisani

Waziri wa maswala ya vijana, sanaa na michezo Kipchumba Murkomen  amedokeza kuwa uwanja unaokaribia kukamilika kujengwa wa Kirigiti, utabadilishwa jina.

Waziri Murkomen amesema kuwa uwanja huo ni wa kihistoria tangu jadi za ukoloni kwani rais wa kwanza wa Kenya Mzee Jomo Kenyatta alihutubia umaa kwa mara ya mwisho kabla ya kukamatwa na kuzuiliwa katika gereza la Lokiatang.

Uwanja huo baada ya kukamilika, waziri Murkomen amedokeza kuwa jina lake litabadilishwa na kuitwa 'Freedom Stadium'. 

Aidha, kabla ya kubadilishwa kwa jina hilo. umma utashirikishwa kutoa maoni ya kufanya mageuzi hayo.

Kwa sasa, uwanja huo unajulikana kama Kirigiti na langoni kumeandikwa 'Krigiti International Stadium'.

Murkomen alidokeza hayo wakati wa kukagua ujenzi wa uwanja huo ambao umejengwa kwa zaidi wa miaka 4.

Hata hivyo waziri Murkomen alisema kuwa aliridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa uga huo akiashiria kuwa na mambo machache yamesalia ili uga huo kuanza kutumika.

Kulingana na Murkomen, uwanja huo utakuwa huru kwa kukuza vipaji vya vijana hivyo basi utaitwa Freedom kuashiria juhudi za waanzilishi wa taifa la Kenya kutumia uwanja huo kufanya mikutano ya kutafuta uhuru wa Kenya.

 

View Comments