In Summary

• Bayern Munich imeshinda mechi tatu za mwisho kwa zaidi ya mabao matano katika ligi ya Bundesliga na ligi ya UEFA.

• Kocha Vincent Kompany anaendelea kujidhihirisha kuwa anaweza kuimarisha viwango vya soka vya Bayern Munich licha ya kukashifiwa kuwa hawezi.

Allianz Arena uwanja wa nyumbani wa Bayern Munich
Image: X// Bayern Munich

Kocha Vincent Kompany anazidi kuendeleza msururu wa kushinda mechi kwa mabao mengi na timu ya Bayern Munich.

Bayern Munich imefunga mabao ishirini katika mechi tatu mfululizo ndani ya siku saba; moja ya klabu bingwa barani Ulaya na mbili za ligi kuu Ujerumani - Bundesliga.

Mnamo tarehe 14 Septemba, Bayern waliwacharaza Holstein Kiel mabao sita kwa moja katika ligi ya Bundesliga.

Siku tatu baadaye, msururu wa kufunga mabao mengi uliendelezwa na Bayern kwa kuwachabaanga Dinamo Zagreb jumla ya mabao tisa kwa mawili.

Kichapo hicho kwa Dinamo Zagreb kiliifanya Bayern Munich kuwa timu ya kwanza barani Ulaya kufunga mabao mengi katika ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.

Bayern ilifikisha jumla ya idadi ya mabao ishirini katika mechI ya ligi dhidi ya Werder Bremen mnamo tarehe 21 Septemba kwa kufunga mabao matano ugenini.

Ubora wa kocha Vincent Kompany umedhihirika licha ya washikadau wa soka kubashiri kuwa ukubwa wa Bayern Munich kihistoria ungemlemea kocha huyo.

View Comments