In Summary

• Mchezaji huyo alianza taaluma ya kucheza soka katika timu ya vijana ya Real Madrid alikofanya vyema na hatimaye kupandishwa kwa timu ya Real Madrid C.

Image: X//Real Madrid

Kifungua mimba wa mwanasoka nguli duniani Zinedine Zidane ametangaza kustaafu kucheza kandanda kitaaluma akiwa na umri wa miaka 29 pekee.

Enzo Zidane, amekuwa na wakati mgumu katika taaluma akijaribu kupata nafasi ya kucheza katika ligi kuu za barani Ulaya.

Zidane ,29, akitangaza kustaafu kwake kwa wanahabari, amesema kuwa kushinda taji kama vile la michuano ya Ulaya hudhibitisha mtu kuwa mchezaji na anafurahia mambo aliyoweza kufanikisha wakati akiwa mchezaji.

"Ukweli ni kwamba ilikuwa nzuri kwangu. Kila wakati nikifikiria mechi zote nilizochezea timu ya taifa sijapeana sababu ya kutosha ya kujishuku. Ukweli nafurahia kila kitu tulichopata."  Alisema Enzo Zidane.

Aidha kulingana na shirika moja la habari nchini Uhispania, Enzo aliamua kustaafu kwa ugumu wa kupata fursa ya kuendelea kucheza kabumbu kwa kuwa nje kwa takribani msimu mmoja.

Mchezaji huyo alianza taaluma ya kucheza soka katika timu ya vijana ya Real Madrid alikofanya vyema na hatimaye kupandishwa kwa timu ya Real Madrid C.

Pia, Enzo alicheza chini ya babake akiwa kocha wa Real Madrid ambapo alifunga bao katika mchuano wa Copa Del Rey dhidi ya Cultural Leonesa ugani Santiago Bernabeu.

View Comments