In Summary

• Timothy Ouma amefungia IF Elfsborg mabao mawili na kutoa assist mbili katika mechi 18 alizochezea klabu hiyo.

• Timu kadhaa zinazoshiriki ligi kuu Italia zinamuwinda kutokana na ubora wake.

Timothy Ouma
Image: X// IF Elfsborg

Kiungo mkabaji wa timu ya taifa Harambee Stars Timothy Noor Babu Ouma maarufu kama Timothy Ouma sasa anavutiwa na timu kadhaa zanazoshiriki ligi kuu Italia, Serie A.

Kinda huyo wa miaka 20, kwa sasa anatumikia timu ya Elfosborg inayoshiriki ligi ya Allsvenskan nchini Uswidi.

Kwa mujibu wa mtaalam wa uhamisho wa soka Gianluca Di Marzio amesema kuwa Empoli ni mojawapo wa vilabu nchini Italia vinavyommezea mate mchezaji huyo.

Empoli  kwa sasa inashikilia nafasi ya tano   kwa alama 9 baada ya michezo tano ya ligi kuu Italia, Serie A msimu huu.

Jumatano 25, Timothy Ouma aliifungia IF Elfsborg bao moja la ufunguzi katika dakika ya 23 kwenye mechi ya ligi ya Ulaya dhidi ya AZ Alkamaar. Mchuano huo uliisha kwa Elfsborg kushinda mabao 3 kwa 2 licha ya kupata kadi nyekundu.

Timothy amekuwa katika fomu nzuri katika ligi ya Allsvenskan na ligi ya Ulaya.

Katika mechi saba alizocheza kwenye ligi ya Ulaya,Timothy Ouma amefunga goli moja, Pia, kwenye ligi kuu Uswidi, ndani ya mechi 17 Ouma amefunga bao moja na kutoa assist moja.

View Comments