In Summary

• Manchester United wana kibarua katika uwanja wa nyumbani watakapocheza dhidi ya Tottenham siku ya Jumapili saa kumi na mbili na nusu.

Image: Premier League

Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL inaingia raundi ya sita ya msimu 2024/2025 wikendi ya tarehe 28 na 29 mtawalia kwa jumla ya mechi  tisa.

Jumamosi 28, Newcastle itakuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester City watakaokosa kiungo cha kati Rodri katika mechi ya mapema mwendo wa saa nane na nusu adhuhuri. 

Siku hiyo, mwendo wa saa kumi na moja jioni jumla ya michuano tano itagaragazwa katika viwanja mbali mbali.

Chelsea ikiwa nyumabni inalenga kuendeleza msururu wa matokeo bora watakapomenyana na Brighton. Brentford watakuwa wenyeji wa West Ham wakati Crystal Palace  watasafiri kucheza dhidi ya   Everton.

Vile vile, Nottingham Forest watacheza na Fulham wakati vijana wa Mikel Arteta Arsenal watacheza nyumbani ugani Emirates dhidi ya Leicester City.

Wolverhampton watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya miamba wa soka Liverpool mechi itakayong'oa nanga saa moja na nusu jioni.

Jumapili 29, itakuwa zamu ya mashetani wekundu Manchester United wakilenga kuimarisha matokeo yao ya ligi watakapomenyana na Tottenham Hotspur wa saa kumi na mbili unusu.

Mechi ya kwanza Jumapili itakuwa kati ya Ipswich town na Aston Villa mwendo wa saa kumi kamili.

Raundi ya sita ya EPL, itakamilika mnamo Jumatatu 30 Bournemouth watakapowaalika Southampton mwendo wa saa nne usiku.

View Comments