In Summary

• Kuanzishwa kwa michezo katika kambi za wakimbizi, kulingana na Murkomen ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuwahamasisha  wakimbizi katika jamii ya Kenya.

• Katika kambi za wakimbizi za Daadab, Kakuma na Kalobeyei, vijana ambao ni wakimbizi wamewezeshwa kupitia mawasiliano ya habari zinazobadilisha maisha yao.

Mji wa kakuma kwenye kaunti ya Turkana
Image: YouTube (screenshot)

Waziri wa maswala ya vijana, sanaa na michezo Kipchumba Murkomen amesema kuwa wizara ya michezo itaanzisha michezo mbali mbali katika kambi za wakimbizi nchini.

Waziri Murkomen alisema hayo katika hafla ya kuwatuza watengenezaji wa filamu kutoka kambi za wakimbizi zilizoko nchini.

Kuanzishwa kwa michezo katika kambi za wakimbizi, kulingana na Murkomen ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuwahamasisha  wakimbizi katika jamii ya Kenya.

Murkomem alisema kupitia mpango wa kutoa fursa za kitaifa za vijana kuelekea maendeleo (NYOTA) vijana wanaoishi katika kambi za Daadab, Kakuma na Kalobeyei watapata fursa  mpango huo utakapozinduliwa katika kambi hizo.

 Aidha Murkomen amesifia shirika lisilokuwa la kiserikali la FilmAid Kenya kwa kuwezesha vijana ambao ni wakimbizi kupitia mawasiliano ya habari zinazobadilisha maisha yao.

Vijana kutoka jamii ya wakimbizi walio katika kambi za Kakuma na Daadab ndio watakuwa wa kwanza kufaidika na mpango wa NYOTA pindi  utaanzishwa katika kambi za wakimbizi.

NYOTA ni mpango kwa vijana kati ya miaka 18-35 katika kaunti 47 unaolenga kukuza mazingira ya vijana kustawi katika taaluma zao.

Wizara ya michezo inatarajia kupitia mpango huo, kuongeza ujuzi wa vijana katika soko la ajira kwa kutoa mafunzo ya kazi, kubuni nafasi za kazi  na kuziba pengo la elimu pamoja na kuziba pengo la ukosefu wa ajira kwa maelfu ya vijana nchini.

View Comments