In Summary

•Mutugi alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilivunjika mwaka wa 2022 wakati mkewe alimuacha kwa sababu ya tabia yake ya ulevi.

•"Ni pombe walikuwa wanakorofishana sana kuhusu. Nitaongea na msichana," Mama Nyambura alisema.

GIDI NA GHOST
Image: RADIO JAMBO

Moses Mutugi ,33, kutoka Chogoria alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Winfred Nyambura ,27, ambaye alikosana naye miaka miwili iliyopita.

Mutugi alisema ndoa yake ya mwaka mmoja ilivunjika mwaka wa 2022 wakati mkewe alimuacha kwa sababu ya tabia yake ya ulevi.

Aliomba kusaidiwa kumrejesha nyumbani mkewe, akibainisha kwamba tayari amebadilika na kuacha pombe kabisa.

"Tulikosana na mke wangu juu ya mimi kuwa mlevi. Nilikuwa natumia pombe sana. Nilikuwa nataka nimuombe msamaha juu niliachana na pombe na ninaendelea sawa. Tumekuwa tukiongea, mara nyingine ananikataa, saa zingine anasema anataka kurudi. Sasa hivi ako Ntugi, Meru.Nimewahi kuenda kwao lakini akakataa kurudi. Aliniambia siku atarudi ataniambia. Nilienda kazi kurudi nikapata ameniachia kijana akaenda. Huwa ata hapigi simu. Mtoto ako kwa nyanyake," Mutugi alisimulia.

Alidai kwamba tayari ameingia katika huduma ya kanisa baada ya kuacha pombe miaka miwili iliyopita.

"Niliacha pombe sasa hivi mimi nachezanga vinanda kanisani na mimi ni mwalimu wa Sunday school. Niko na miaka miwili tangu niache pombe," alisema.

Gidi aliweza kumpata Mama Nyambura ambaye alithibitisha kwamba bintiye aligura ndoa yake kutokana na pombe.

Hata hivyo, aliahidi kuzungumza na bintiye ili kuona kama ataweza kurudi katika ndoa yake.

"Ni pombe walikuwa wanakorofishana sana kuhusu. Nitaongea na msichana," Mama Nyambura alisema.

"Acha nitaongea na Nyambura nikwambie mambo kamili. Msichana ndiye ataamua,' alimwambia Mutugi.

Mutugi alisema, "Anisamehe, arudi nyumbani. Nimeachana na mambo ya pombe kabisa. Ata sitakaribia mahali inauzwa."

Je, una maoni ama ushauri upi kuhusu Patanisho ya leo?

View Comments