In Summary

•Njoroge alisema shida ilianza baada ya mtoto wao kuaga ambapo baadaye mkewe alimlalamikia kwa kukataa ombi lake.

•Janet aliweka wazi wazi kwamba hawezi kurudiana na Njoroge na kudai kwamba hakuwa akiwajibika nyumbani.

Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kitengo cha Patanisho, jamaa aliyejitambulisha kama Nahashon Njoroge ,38, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mkewe Janet Wanjiku ,40, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Njoroge alisema ndoa yake ya zaidi ya mwaka mmoja ilisambaratika Mei mwaka huu wakati  mkewe aliondoka.

Alisema shida ilianza baada ya mtoto wao kuaga ambapo baadaye mkewe alimlalamikia kwa kukataa ombi lake.

"Nilikuwa nafanya kazi pande za kwao Kiambu. Tukajuana na tukapanga kuoana. Ilikuwa 2021, alafu tukaunganishwa na pasta wangu 2022. Baadaye tukaenda nyumbani, alafu nikaenda kazi mahali kwingine," Njoroge alisema.

Aliongeza, "Nilikuwa nimemuoa akiwa na msichana wa form 2. Tulibarikiwa na mtoto alafu akaaga mwaka jana mwezi wa pili. Baadaye tumekuwa tukivutana. Alipata kazi alafau  akasema alikuwa amezidiwa sana na kazi, na ati sikuwa natoa chochote kwa nyumba. Tulikuwa tunasaidiana. Aliambia babangu anataka kuenda, anataka kupewa ruhusa ya kuchukua nguo. Alipanga virago vyake, akaenda mwezi wa tano. Alikuwa anasema nasikiliza mamangu sana."

Njoroge alisema amekuwa akionana na mkewe kanisani ila hawajakuwa wakizungumza licha ya kujaribu kupatanishwa.

"Amekuwa akija kanisani lakini hatuongei. Tumejaribu kuongea na mchungaji na mzee wa kanisa lakini imeshindikana. Ningependa turudiane kwa sababu anajua shida zangu za mwili na ameweza kunikubali nilivyo. Nakuwanga na ugonjwa wa kifafa," alisema.

Janet alipopigiwa simu, aliweka wazi wazi kwamba hawezi kurudiana na Njoroge na kudai kwamba hakuwa akiwajibika nyumbani.

"Mimi siwezi. Wakati tulioana, hakuwa anatimiza matumizi ya nyumba," alisema kabla ya simu kuwa na matatizo.

Je, ushauri ama maoni yako kuhusu Patanisho ya leo ni yepi?

View Comments