AMREF, Juliani kuhamasisha vijana kuhusu Covid-19

images (5)
images (5)

Juhudi za kupambana na covid 19 nchini zimepigwa jeki kufuatia kuundwa kwa miradi ya uhamasisho inayoongozwa na vijana.

Shirika la Amref limeshirikiana na mwanamziki maarufu Juliani kupitia vuguvugu lake la Dandora Hip Hop City kuwapa mafunzo vijana 150 kuhusu jinsi ya kusambaza maarifa kuhusu maradhi haya kwenye mitaa na pia mitandaoni.

Hayo yakijiri, balozi wa Marekani Kyle McCarter ametoa msaada wa maski elfu 40 kwa polisi wanaoshika doria mipakani ili kuwasaidia kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Kenya imefunga maeneo yanayopakana na Tanzania na Somalia kama njia ya kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Kwingineko, unywaji pombe haramu kwenye mabaa mjini Eldoret umesalia kuwa changamoto kubwa inayohujumu juhudi zinazoendelea za kudhibiti maambukizi ya Corona. Kamishna wa polisi eneo hilo Abdirisack Jaldesa anasema licha ya wao kujaribu kukomesha uuzaji wa pombe hiyo, baadhi ya vijana wangali wanapuuzilia amri ya kutotangamana na kukusanyika katika mabaa ya chang’aa.