Anachotakiwa kufanya Ruto kabla 2022. Apinge au aunge mkono serikali kuhusu Mau?

Mchakato wa kuhamisha familia zinazoishi katika msitu wa Mau ni kati ya maswala yanayomkosesha usingizi naibu wa rais William Ruto. Hili ni zoezi ambalo serikali inapania kutekeleza ili kulinda msitu ambao ni usuli wa maji.

Inafahamika kwamba idadi kubwa ya wananchi wanaishi katika eneo hili na ni tishio kubwa kwa mazingira iwapo ukataji miti ya ujenzi utaendelea. Aidha ukataji miti katika harakati za kutayarisha mashamba ni tishio kubwa linaloweza sababisha ukavu.

Soma hadithi nyingine hapa:

William Samoei Ruto sasa amesalia katika njia panda. Aidha aunge mkono swala nzima na mpango wa serikali au akaidi na kuikashifu serikali katika nia ya kuwafurusha raia katika msitu huu. Hili lina faida kubwa kwani ni njia moja ya kuwa kipenzi cha wapiga kura 2022.

Kizungumkuti kinamkuta pale ambapo anatakiwa kuunga mkono azma ya serikali kuulinda msitu huu ama kuipinga serikali ili avutie upatu mkubwa katika uungwaji mkono 2022.

Soma hadithi nyingine hapa:

 Uhamisho wa wananchi katika msitu huu ni mtihani mkubwa sana kwa Ruto. Ikumbukwe kuwa Ruto amenukuliwa na vyanzo mbalimbali akisema kuwa yeye ni "Mtu wa mkono wa Rais". Kwa kauli hii anatakiwa kuwa katika mstari wa kwanza kuidhinisha hili zoezi.

Swala la kuutetea msitu huu ambao ndio chimbuko kubwa zaidi nchini la maji limekuwa dondasugu na kupelekea kuwalaani wanasiasa wengi nje na ndani ya mipaka ya bonde la ufa.

Soma hadithi nyingine hapa:

“Ruto yupo kwenye kizungumkuti. Uhamisho wa raia msitu wa Mau unakuwa na uhasama na utasalia kuwa hivyo. Jinsi atakavyosuluhisha utata wa zoezi hili utategemea iwapo atakuwa rais wa tano wa nchi hii au atauma nje,"  Mchanganuzi wa siasa Herman Manyora

Ruto ambaye tayari ashaweka wazi nia yake ya kumrithi Uhuru Kenyatta 2022 sasa anatembelea katika ardhi tepetevu. Jinsi na ambavyo atatatua swala hili ni kipengele muhimu kitakachoamua kuwa atapata atamrithi au atakosa kiti hiki.