Apokea hela kimakosa M-Pesa. Aburuzwa kortini kujibu mashtaka ya wizi

unnamed__1568966760_23858
unnamed__1568966760_23858
Jamaa aliyetumiwa pesa kimakosa kupitia huduma ya M-Pesa sasa yuko mashakani.

Stanley Irungu alipokea elfu 60 kutoka kwa mwanamke mfanyabiashara.

Irungu ameshtakiwa kuwa Juni 22 katika mtaa wa Umoja alihusika katika kitendo cha wizi.

Soma hadithi nyingine:

Hela hii ilikuwa ya Millicent Atieno.

Polisi wanahoji kuwa Atieno ambaye ni muhudumu wa M-Pesa Umoja alipatiwa pesa na mteja aweke katika akaunti yake.

Atieno alituma kitita hiki cha pesa kwa akaunti ya Irungu kimakosa.

Irungu ameshtakiwa kutoa kiwango cha hela 39,000.

Atieno alipigia kampuni ya Safaricom ili kurudisha elfu 21 zilizosalia katika akaunti ya Irungu.

Atieno alijaribu kumpigia simu Irungu bila mafanikio.

Soma hadithi nyingine:

Kisa hiki kiliripotiwa katika kituo cha polisi na baadaye akakamatwa.

Irungu alikubali kupokea elfu 60 na kusema kuwa yupo tayari kurudisha hela hiyo.

"Nilipokea pesa hizo na nikatoa kiwango kidogo. Nipo radhi kumlipa Atieno hela zake." Irungu aliiambia mahakama.

Mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya elfu 20. Kesi hii itatajwa Oktoba 1.