Fred.arocho na.mkewe. ufaransa

Arocho na mkewe Sophie washeherekea fungate ya pili Ufaransa

Ikifikia ni mambo ya mapenzi na jinsi ya kulewesha mkewe kwa upendo na mahaba, basi mtangazaji Fred Arocho anaongoza katika sehemu hiyo.

Mtangazaji huyo mahiri wa soka nchini, sasa hivi yuko Ufaransa ambako amempeleka mkewe, bi Sophie, akajivinjari katika fungate (honeymoon) yao ya pili miaka kumi tangu wawili hao walipo funga ndoa.

Arocho takes 10 cows to in-laws to commemorate a decade in Marriage

arocho na sophie

Safari hiyo ya kipekee inawadia miezi kadhaa tangia Arocho alipo wazawadi wakwe zake ng’ombe kumi, kuashiria miaka ambayo ameishi na mwana wao katika ndoa.

Wapendwa hao wawili wamejaliwa wana wanne, msichana mmoja na vijana watatu.

Arocho reveals how he lost Sh5,000 for failing to identify his wife

fred.arocho.and.wife

Fungate hii ya Ufaransa inaashiria jinsi wawili hawa bado wanaogelea pamoja katika bahari la mapenzi.

Tukizungumza na gwiji huyu anayetambulika kama bwana Laduuma, alifichua kuwa katika likizo yake ndogo, anapania kuyazuru maeneo tofauti yanayotambulika kote duniani.

“Kabla turudi nyumbani, mimi na Sophie tunapangia kuzuru mnara wa Eiffel (Eiffel tower) jumba la Versailles, miji ya Marquise, Saint Yon, Boussy na pia kuzuru uwanja wa timu ya soka ya PSG.” Alisema Arocho ambaye alikuwa na wingi wa furaha.

arocho na sophie ufaransa

Lakini anacho pania zaidi ni kuzuru daraja la mapenzi (bridge of love) ambapo wapendwa wawili hufunga kufuli zinazo ashiria upendo wao, kisha kutupa funguo ndani ya maji. Kufuli hizo husalia hapo milele na huashiria kuwa upendo wao ni wa milele.

PHOTOS: Fred Arocho and his lovely wife celebrate their birthdays in style

fred arocho ufaransa

Likizo yake pia ili ambatana pia na shughuli zake za uanahabari, kwani amekuwa aki ripoti shughuli za Harambee Stars ambao pia wapo Ufaransa kwa kambi ya mazoezi, huku wakijitayarisha katika kinyang’anyiro cha kombe la mataifa ya Afrika.

fred arocho na Sophie

Katika pilka-pilka hizo, aliweza kuwa na mahojiano ya moja kwa moja na nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama na kocha Sebastien Migne.

arocho na Wanyama

Tunawatakia wapendwa hawa wawili kila la heri katika ndoa yao.

Photo Credits: Fred Arocho

Read More:

Comments

comments