Arsenal wainyuka West Ham, baada ya kukosa ushindi katika mechi 9

west ham
west ham
Arsenal imejikokota na kujipa ushindi licha ya kushindwa kwenye misurururu ya mechi 9. Hii Ni baada ya kupiga West Ham mabao 3-1 ukiwa ndio ushindi wa kwanza chini ya uongozi wa kaimu mkufunzi Freddie Ljungberg.

Bao la kwanza lilitingwa na Gabriel Martinelli mwenye umri wa miaka kumi na minane  na kusawazisha baada ya Angelo Ogbonna kufungia West Ham katika kipindi cha kwanza ugani London.

La pili lilifungwa na Nicolas Pepe dakika 9 baadaye kupitia mkwaju wa kona huku la tatu likitingwa na Pierre-Emerick Aubameyang. Ushindi huo uliisogeza Arsenal hadi nafasi ya 9 ligini.

Meneja wa Chelsea Frank Lampard amemjumuisha Antonio Rudiger kikosini kuikabili Lille kwenye ligi ya primia huku akimwacha nje Fikayo Tomori.

Tomori hakuchezeshwa Kama mchezaji wa akiba kwenye mchuano dhidi ya Everton ambapo waliwalaza mabao matau kwa moja. Aidha, mchezaji huyo wa Uingereza hatasakata mechi ya leo kutokana na jeraha la paja.

Chelsea wanafaa kuibuka kidedea ili kuiweka katika nafasi bora kwenye jedwali.

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ameambiwa kwamba kazi yake iko salama na mmiliki wa klabu hiyo na kwamba hawatamuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino.

Wakati huo huo, Manchester United wana mpango wa kumpatia kiungo wa kati wa Uskochi mwenye umri wa miaka 23 Scott McTominay mkataba mpya wa pauni elfu 60 kwa wiki.

Harambee Stars itamenyana leo na Sudan kwenye mechi yao ya pili ya kombe la CECAFA, na endapo watashinda leo, watapenya moja kwa moja hadi kwenye nusu fainali.

Hii ni baada ya kujitwalia ushindi katika mechi yao ya ufunguzi. Aidha, Stars hawataongozwa na Kocha wao Francis Kimanzi ambaye alipigwa marufuku na CECAFA kutokana na masuala ya kinidhamu.

Kimanzi na naibu wake Zedekiah Otieno wanadaiwa kuchochea Stars wakatae kucheza na Tanzania kutokana na tetesi kwamba wachezaji watatu wa timu hiyo hawakuwa na paspoti halali. Kadhalika, wanadaiwa kuwafukuza maafisa wa michezo kwenye chumba cha kuvalia sare.