Arsenal wako tayari kumwachilia Laurent Koscielny

koscielny
koscielny
Arsenal wako tayari kumwachilia Laurent Koscielny kuondoka klabuni humo iwapo tu hesabu yao itaafikiwa.

The Gunners wameanza mchakato wa kinidhamu dhidi ya Koscielny baada yake kudinda kusafiri na timu hiyo kwa ziara ya kabla msimu kuanza nchini Marekani.

Koscielny amesalia na mwaka mmoja katika mkataba wake na anataka kuwachiliwa huru ili aweze kuregea Ufaransa.

Alijiunga na Arsenal kutoka Lorient mwaka wa 2010 na amechezea klabu hio ya ligi ya Primia mara 353.

Kieran Trippier wa Tottenham anakaribia kukamilisha uhamisho kuelekea Atletico Madrid. Kiungo huyo wa Uingereza ataekelea Uhispania hii leo ambapo atafaniwa uchunguzi wa kimatibabu, huku mazungumzo kuhusu mkataba akiendelea.

Kama sehemu ya majadiliano ya mkataba wa  Trippier, Tottenham wamepewa fursa ya kumsajilii mshambulizi wa Atletico Madrid Angel Correa. Haijabainika iwapo Spurs wanamtaka Correa lakini ni muargentina na anatambuliwa vyema na Mauricio Pochettino.

Kiungo wa Barcelona Philippe Coutinho mwenye umri wa miaka 27, huenda akarejea Liverpool kwa mkataba wa miaka miwili kwa mkopo, huku timu hiyo yenyewe ikiwa na mipango ya kumnunua kwa pauni milioni 88. Kwingineko Bayern Munich imekata matumaini ya kumalizia mkataba wa pauni milioni mmoja kumnasa winga wa Manchhester City Leroy Sane, mwene umri wa miaka 23.

Kinda huyo wa miaka 19 ambaye alikua amehusishwa na Manchester United, Barcelona na Paris-St Germain, aliwaongoza miamba hao wa Dutch hadi kwa nusu fainali ya ligi ya mabingwa msimu uliopita. De Ligt alianza kuchezea Uholanzi Machi mwaka wa 2017 licha ya kuanza mechi mbili tu akiwa Ajax wakati huo.