Asanteni wote! Anerlisa Muigai amewashukuru watu wote walioombea familia yao

Anerlisa Muigai ambaye hivi maajuzi alifunga pingu za maisha na mpenziwe Ben pol katika harusi ya kisiri amewashukuru wale wote waliosimama na familia yao baada ya kumpoteza dadake Tecra Muigai

Kama njia ya kuonyesha upendo kwa Tecra, Anerlisa alitumia fursa hiyo kutundika picha za dadake huyo wakiwa pamoja na kufuatisha ujumbe kuwa atamkosa saana baada ya kifo kumyakua.

Kwake, Tecra alikuwa kama mwanga wake na furaha ya moyo wake.

Tecra alifariki mnamo Mei 2, 2020 kutokana na jeraha baya la kichwa lililotokana na kuanguka kutoka kwa ngazi ama stairs.

"She knew I did not like to show my arms so she told me this cardigan would suit me. I loved it," Anerlisa  alimsifia dadake Tecra.