Asanteni wote mliofanikisha uzinduzi wa Albamu yangu,asema Harmonize

pjimage (12) (1)
pjimage (12) (1)

NA NICKSON TOSI

Masaa machache tu baada ya kuzindua albamu yake mpya ya AFROEAST,Harmonize amewapongeza wote waliofanikisha kazi yake hiyo aliyoifanya wikendi.

Katika posti yake ,Harmonize ameelezea kuridhishwa jinsi watanzania waliovyojitokeza na kuhudhuria uzinduzi huo hadi usiku wakiwemo rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete.

“Licha Ya Yote....!!! Yaliyotokea Jana...!!! Furaha Yangu Ilikuwa Kumuona Mzee Wangu Amekaa Mlimani City Mpaka Saa 8:30 Usiku Daah..!!! 😭😭😭 Mungu Akubariki Sana...!!!  Jakaya Mrisho Kikwete 🙏 Pamoja Na Viongozi Wote Wa Serikali ,Naibu Spika ,Waziri Mwenye Dhamana...!!! wa Michezo Doctor Harison Mwakyembe ...!!! Na Watanzania Wote..!! 🙏🙏🙏🙏🙏aliandika Harmonize