Asenal yamkashifu nahodha wao Laurent Koscielny

koscielny
koscielny
Nahodha wa Arsenal Laurent Koscielny amekataa kujiunga na kikosi cha Arsenali kwa mechi za maandalizi ya msimu mpya mjini Los Angeles nchini Marekani.

"Tumesikitika sana na matendo ya koscielny ambayo ni kinyume na matarajio yetu pamoja na maagizo ya klabu. Tunatarajia kusuluhisha jambo hili haraka iwezekanavyo," Arsenal imesema.

Arsenali inatarajiwa kung'o nanga hii leo kuelekea Marekani ambapo itachuana na Colorado Rapids, Bayern Munich,Fiorentina pamoja na Real Madrid.

Awali wiki hii klabu ya P.S.G iliamua kumuadhibu mshabulizi wake Neymar baada ya kudinda kurudi mazoezini kama ilivyo kwa matarajio ya klabu. Pia,Klabu ya Atletico Madrid iliamua kuifungulia Barcelona na mshambulizi wake Antoinne Griezmann mashtaka kwa kukataa kujiunga na klabu kama ilivyo tarajiwa.