Asha Mwilu mtangazaji mpekuzi atangaza kuihama runinga ya Citizen

VGiRuhDC.jfif
VGiRuhDC.jfif
Mwanahabari  mpekuzi Asha Mwilu ametangaza kuihama televisheni ya Citizen baada ya kuhudumu pale kwa muda  kwa kile amesema ni kwenda kufungua kampuni yake ya kibinafsi.

Alijiunga na runinga hiyo mwaka 2018 na amefanya makala mengi yakiwemo Mara Heist, makala yaliyokuwa yanaangazia wizi katika chuo kikuu cha Masai Mara.

''Some personal news: I'm leaving to launch my start-up. I've worked under the guidance of the brilliant poeple'' aliandika Asha katika mtandao wake wa Twitter.

Mwilu vile vile aliwashukuru wanahabari wenzake Pamela Asigi, Linus Kakai na Joy Ageyo kwa wakati mzuri waliokuwa nao wakifanya kazi kwa pamoja.