Askofu Deya stadi wa "kiingeresha" amfunza Massawe!

Mtangazaji Massawe anayefanya kipindi cha Bustani la Massawe katika kitengo cha Ilikuaje huwahoji wageni tofauti tofauti katika studio. Wiki hii akaja Askofu mwenye utata Gilbert Deya ambaye kwa kuwa ameishi Uingereza kwa miaka 15 akawa anajinadi na kujipiga kifua kuhusu uweledi wake wa lugha ya kiingereza.

Pata hadithi hapa:

Deya ni mhubiri tata aliyewahi kugonga vichwa vya habari kwa umaarufu wa kuwaombea wanawake na baadaye kupokea baraka za watoto almaarufu kama "Miracle babies". Katika kipindi hiki, Gilbert alitangaza kuwa haoni tatizo Askofu Ng'ang'a kuwatusi na kuwakaripia watumishi wake pale kanisani.

Katika mahojiano yaliyochukua saa moja, Massawe alimuuliza kuhusu tetesi kukua aliwahi kuhamishwa kwa nguvu kutoka nchi ya Uingereza hadi nchini kwa tuhuma za kuiba mtoto. Ikumbukwe kuwa, raia wa nchi tofauti anapohitilafiana na sheria katika nchi nyingine anaweza kufurushwa nchini humo. Tendo kama hilo kwa kiingereza huwa ni "Deportation." 

Soma pia:

Neno hili kulingana na Deya halikufaa kitendo hicho kilichotekelezwa na serikali ya Uingereza. Kulingana naye, Massawe angefaa kusema "Extradited". Neno hili la kiingereza likiwa na maana kuwa mshukiwa alitumwa nchi aliyofanya uhalifu akashtakiwe huko ambayo ni Kenya.

"Rumour has it that you were deported, is it true?" aliuliza Massawe.

"No, it's not Deportation, you don't know English, jaribu kishwahili... i was extradited...its different from deportation." alijitetea Deya.

"Now  that you know English than myself, whats the difference?" Aliuliza Massawe.

"Sasa wewe ni Swahili yako unanipinga nayo...Mimi nilikuwa extradited nikuje nianze kesi hapa Kenya. Nikimaliza keshi Nitarudi Uingeresha... Unajua kiswahili ni hatari kwangu kama vile wewe kizungu inakusumbua."

Soma pia: