Askofu wa kanisa la kikatoliki auwawa baada ya kudungwa kichwani

Askofu wa kanisa la kikatoliki jimbo la Meru alifariki papo hapo asubuhi ya Jumanne baada ya kudungwa mara mbili kichwani.

Akidhibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi eneo la Imenti kaskazini, Robinson Mboloi alisema kuwa askofu huyo alidungwa katika maeneo ya biashara ya Makutano mida ya 1:45 asubuhi.

“Alikuwa amekodisha chumba cha malazi huku akiwa na mwanadada saa nne unusu usiku baada ya kunywa pombe mchana mzima.” Alisema Mboloi.

Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa Eutycas Murangiri Muthuri mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa anahubiri katika parokia ya Tigania magharibi, alidungwa mara mbili na kufariki papo hapo kutokana na kupoteza damu nyingi.

“Alidungwa utosini na pia kisogo alipokuwa akiabiria gari lake alilokuwa ameegeza nje.”Alisema.

Uchunguzi wa The Star ulibainisha kuwa askofu huyo alienda kuabiri gari lake aina ya Toyota Khami, KBH 972S, mida ya saa saba asubuhi.

Wasimamizi wa maeneo hawakutupa maoni yao kwani walikuwa wanarekodi taarifa na maafisa wa polisi.

Hata hivyo mkuu huyo wa polisi alisema bado wanachunguza kuidhinisha kama askofu huyo alidungwa akiwa nje au ndani mwa gari lake.

“Mshambulizi huyo bado hajatambulika wala wala sababu zake za kumvamia askofu huyo kujulikana lakini mwandada aliyekuwa naye na pia mwanaume ambaye walikuwa pamoja." Mboloi alisema.

Mwili wa mwendazake uko katika nyumba ya kuhifadhi maiti ya hospitali ya Meru level five ukingoja kufanyiwa upasuaji, huku gari lake likiwa katika kituo cha polisi cha Meru.

-Dennis Dibondo