Askofu Wafula afunguka baada ya matusi ya "Lubbish, allogant,idiot"

Baada ya kurushiwa cheche za matusi majuma chache yaliyopita kutoka kwa bosi wao Askofu Ng'ang'a, Wafula amefunguka kwa mara ya kwanza kumhusu kiongozi wao.

Soma hapa:

Wafula ambaye kwa sasa amefungua kanisa lake mjini Mombasa anaonekana kutokuwa na matatizo na kiongozi wao.

James Ng'ang'a aliteka vichwa vya habari kwa kuwatusi askofu wake kwa kile alichokitaja kama hawamheshimu. Kiongozi huyu wa Neno Evangelism Centre iliyopo katikati mwa jiji la Nairobi aliteta kuwa askofu Wafula na wengine walianza pale kanisani wakiwa maskini kabisa.

Soma hapa:

Aidha, alionekana kukasirishwa na jinsi hawampi heshima bibi yake. Wafula amesema haya kumhusu Ng'ang'a.

"Mungu akukumbuke baba yetu popote pale ulipo. Babangu Ng'ang'a tumetembea kwingi na wewe. Nimepata tajriba ya kuongea mbele ya hadhira kupitia kwako. Nakuheshimu sana. Sitawahi kukusahau popote niendapo."

Kanisa lake mpya Wafula linafahamika kama Shalom Miracle Church. Wafula alikuwepo na kongamano na wafuasi wake katika uwanja wa Tononoka mjini Mombasa na kuwahubiria mamia ya waumini.