Ata kama umeokoka, macho huwa hayaokoki-Askofu Deya

Mhubiri tata Gilbert Deya katika kipindi cha Bustani la Massawe kinachoruka kupitia kituo cha Jambo amesimulia mwanzo mwisho kuhusu familia yake na jinsi alivyotengana na mkewe.

Soma hapa:

Askofu huyu pia alifunguka kuhusu tamaa ya mwili na jinsi anajitahidi kuoa mwanamke anayemzidi kwa miaka 50 ili kujiepusha na dhambi ya uzinifu. Deya alisema kuwa yeye hangependa kufanya maswala ya mahusiano kisirisiri.

Kauli tata na ambayo ilionekana kumshangaza mtangazaji Massawe ni aliposema kuwa wanaume wengi kanisani wanajidanganya ni waaminifu katika mapenzi.

Soma hapa:

"Wanaume wana changamoto ya kuona wanawake wazuri. Wanajidanganya wakiwa pale kanisani waonekane watu wazuri. Na ata kama umeokoka, macho hayawezi kuokoka.” alisema Deya

Deya alijitenga mbali na swala nzito la kuombea wanawake wapate watoto wa kimiujiza huku akidokeza kuwa dhana hii potovu inaendeshwa na vyombo vya habari na kumfanya aonekane mbaya.

Mwanamke ambaye Deya anapania kumwoa ana miaka 27. Deya alisema kuwa amewatembelea wazazi wake ili kuweka utaratibu mwafaka wa ndoa.