Atwoli amlimbikizia sifa Raila kwa ustadi wa kupanga mambo!

Raila
Raila

Katibu wa COTU  Francis Atwoli  alimsifia  kinara wa upinzani na kiongozi wa chama cha ODM  na kumtaja kuwa shupavu katika kupanga mikakati ya chochote anachofanya.

Atwoli alikuwa anatoa hotuba ya kumkaribisha Raila kwenye mkutano wa OATUU jijini Nairobi.

''Katika maisha yangu, Raila ndiye mtu ambaye anajua kupanga mambo sana. Waweza kuwa na Raila mpaka saa nane asubuhi na kisha baaadaye ushtukiye kumuona akihudhuria mkutano mbali licha ya uchovu.'' Atwoli alisema.

''Na ndio maana nasema kuwa, una mipangilio mwafaka na hakuna mwanasiasa ambaye anafaa kupewa jina hili''

Atwoli alimsifu Raila kwa zaidi ya robo saa na akazidi kusema kuwa, majina yote ya lakabu ya aliyekuwa waziri mkuu yanamfaa.

Majina haya ni kama Agwambo, Enigma na majina mengine mengi.

''Sisi ambao tunatoka katika mashirika ya kutetea maslahi ya wafanyikazi na makundi ya vuguvugu, tunakuenzi sana na kuiga utendakazi wako .'' Atwoli alisema.

''Babake Obama ametoka kwenye jamii moja na ulipozaliwa  na ndio sababu tuna watu bora kama wewe ambao huleta matokeo bora kwa wote duniani.'' Atwoli alizidi kusema.

Zaidi ya hayo, Raila alisimama na kusema kuwa, kitu ambacho Atwoli amesahau kuwaambia watu  ni kuwa, yeye ni binamu yake Obama.'

''Alichosahau kuwaambia ni kuwa, mimi ni binamuye Obama''