AU yaanzisha mikakati ya kujiondoa ICC

Viongozi wa bara Afrika wameanzisha mikakati ya kujiondoa kutoka mahakama ya kimataifa ya ICC.

Pendekezo hilo liliungwa mkono kwa kauli moja na mawaziri wa maswala ya kigeni wa nchi ambazo ni wanachama wa muungano wa AU. Kenya tayari imewasilisha ombi la kutaka kubadilishwa kwa sheria ya ICC ya mwaka 2008.

Viongozi wa Afrika pia wanataka kusitishwa kwa kesi dhidi ya Naibu rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang zinazowakabili huko ICC.