AUDIO: Ghost Mulee apendekeza Sam Nyamweya ajiuzulu kufuatia madai ya ufisadi

Hivi leo, ripoti zilizuka kwamba rais wa shirikisho la soka nchini Sam Nyamweya anachunguzwa na CID kwa madai ya kutumia stakabadhi bandia ili kupata shilingi milioni 83 kutoka kwa mdhamini wa kimataifa.

Kampuni hiyo ya kibinafasi ilitoa malipo hayo baada ya kutia sahihi makubaliano kuhusu haki juu ya mechi za KPL. FKF ikiongozwa naye Nyamweya wakati huo haikueleza kwamba ilikuwa na mkataba mwingine wa haki juu ya ligi hiyo na kampuni nyingine kutoka afrika kusini.

Kwingineko, kamati ya senate kuhusu leba imepewa miezi miwili kuchunguza madai ya ufisadi na utumzi mbaya wa mamlaka katika shirikisho la soka nchini FKF. Hii ni baada ya seneta wa Nairobi Mike Sonko kuwasilisha stakabadhi zinazo onyesha ufujaji wa mamilioni ya pesa zilizofaa kukabidhiwa vilabu vya ligi kuu ya humu nchini.

Kufuatia ripoti hizi, Ghost Mulee aliyekuwa mkufunzi wa timu ya kitaifa alipendekeza kuwa ingekuwa jambo la busara kama rais wa shirikisho la FKF, Sam Nyamweya angejiuzulu ili kuwapatia wapelelezi nafasi murwa ya kufanya uchunguzi dhidi ya madai hayo ya ufisadi.

Huku akielezea hayo, Ghost alitaja mifano kadhaa ambayo inaashiria shida ambazo zinaikumba timu ya taifa Harambee Stars huku misingi yake ikiwa swala la ufisadi.

Skiza kanda hii, ambapo pia Ghost pia alielimisha taifa kuhusu sheria ambazo zitaiwezesha Kenya kutopigwa marufuku na shirikisho la kandanda duniani, FIFA.

&feature=youtu.be