AUDIO: Hii Unga Ya Mexico Mtu Hashibi Inabidi Uongeze Githeri

16649565_647102085477744_6951482243422551022_n
16649565_647102085477744_6951482243422551022_n
Baada ya wiki mbili ya likizo nchini Ufaransa, mtangazaji Gidi Gidi wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi alikaribishwa na mashabiki chungu nzima nzima ambao walikuwa wamemngoja kwa hamu na ghamu.

Kama kawaidi baada ya habari za saa moja huwa ni wakti wa mada huku watangazaji wakiwapa waskilizaji fursa ya kuchangia mijadala ambayo imegonga vichwa vya habari.

Lakini leo mambo yalibadilika kwani swala la siasa liliwekwa kando kidogo huku wakenya wakiamua kuzungumzia swala la unga wa ugali ambalo limekuwa likizungumziwa kwa mda sasa. Hii ni baada ya serikali kuu kununua mahindi kutoka nchi ya Mexico baada ya nchi kukumbwa na uhaba wa bidhaa hiyo.

Serikali pia ilipunguza bei ya unga wa ugali huku wananchi wakifurahia jambo hilo, huku wengine wakiwa na maoni tofuati kuhusu unga huo huo.

Baadhi ya maoni hayo yaliwakilishwa asubuhi ya leo, lakini ni maoni yake Martin Anangwe, shabiki sugu wa Radio Jambo ambayo yalimfuruhisha na pia kumshangaza bwana Gidi.

Kulingana na Martin, Unga huo unaoaminika kuwa wa kutoka Mexico sio kama ule aliouzoea kwani unakatika katika na isitoshe hauna uwezo wa kumpa yeyote shibe.

"Sasa mimi nitaongelea mambo ya unga. Hii unga niliona jana na sasa huku Kawangware ukinunua unga hufai kununua zaidi ya pakiti tatu." Alisema Martin.

"Unga yenyewe ni extraordinary sio zile unga tumezeoa, ukishapika ugali tena inavunjika vunjika haikai unga ya kawaidi sasa hatujui ni nini kinaendelea." Aliongeza Martin kabla ya kusema kuwa lazima uongeze Githeri ili uweze kulala.

Pata uhondo kamili.