AUDIO: Jubilee Wako Pamoja Kula Nyama Tu, Asema Isaac Rutto

isaac-rutto
isaac-rutto
Gavana wa Bomet, Isaac Rutto alizuru studio za Radio Jambo siku ya Jumatatu, 26/9/2016 ambapo alizungumzia maswala mengi ya kisiasa na maendeleo swala moja likiwa la minofu ya 'nyama' ambayo rais Uhuru Kenyatta alikiri kuwa serikali ya Jubilee inafurahia.

Gavana Rutto ambaye amekuwa kwenye vyombo vya habari kwa maswala mengi, mojawapo ikiwa uhusiano wake na naibu wa rais, William Ruto, maoni yake kuhusu uongozi wa Jubilee na pia chama chake kijulikanacho kama 'Chama Cha Mashinani' ambacho anasema kuwa kinahusika na mambo yanayowakumba wananchi wa kawaida.

Isisahaulike kuwa Rutto karibu wapigane na kiongozi wa walio wengi bungeni, Aden Duale wakti Duale alipomkashifu mwenzake kwa kufyonza fedha za umma huku akimshutumu kuwa "Pesa si za mamako".

Akizungumzia uhusiano wake na William Ruto, gavana huyo alidai kuwa lengo la kuunda chama cha mashinani halikuwa la kupimana nguvu na Ruto.

"Mimi sitaki kuwa naibu wa rais, hata nikitaka nitahitaji cheo cha rais. Sisi hatupimani nguvu mimi tukisikizana mambo yanayohusisha raia hatuna shida." Alisema Rutto.

"Hivi majuzi walipopanda juu waligeuka sana, ile mambo tuliagana na TNA ya asilimia 40 ya rasilimani kuelekezwa mashinani wakageuka hayo" Aliongeza.

Huku akizungumzia swala la 'nyama' na chama cha Jubilee, Rutto adai kuwa chama hicho hakina sera kamili na nia yao tu ni kuleta watu pamoja kula nyama na yule hatajiunga nao atabaki kunusa tu.

"Hebu nieleze Jubilee iko na sera gani wanakuambia wanataka tuwe pamoja, tuko pamoja kufanya nini? tuko pamoja kula nyama bana na wewe kama hauko nasi basi hauli nyama wewe nusa tu na umeze mate." Alikiri Rutto.

Skiza kanda ifuatayo upate mahojiano yote naye gavana wa Bomet.

&feature=youtu.be