AUDIO: Mateso Na Shida Alizopitia Evelyn Muthoka Zawaacha Wengi Wakibubujikwa Na Machozi

evelyn.muthoka
evelyn.muthoka
Wengi hawakuwa na ufahamu walipoliskia jina lake leo asubuhi, lakini pindi tu msanii Evelyn Muthoka alipoanza kusimulia ushuhuda wake, aligusa nyoyo za milioni za wakenya wengi ambao wamepitia au wanapitia shida kama zake.

Bi. Muthoka ni msanii wa nyimbo za injili na umaarufu wake ulianza kutamba tangia alipozindua kibao chake; 'Digital' ambacho kinawalenga sana vijana.

Kando na kibao hicho, ana kanda kadhaa ambazo zinajumisha nyimbo kama; 'Shetani hauna mamlaka' 'kimbelele' na pia 'Adui yako msamehe'.

Kando na nyimbo zake, masaibu aliyoyapitia bi. Muthoka ndiyo yaliyowagusa na hata kuwapa moyo waskilizaji wa Radio Jambo wengi wao ambao walikiri kuwa, huenda ikawa ndio mahojiano bora zaidi washawahi pata fursa ya kuskiza katika stesheni yetu kwa mda mrefu.

Alianza taaluma yake ya uimbaji mwaka wa 2009 huku uchungaji ukianza mwaka uliopita, lakini kando na wengi ambao huanza uimbaji wakiwa wamekomaa, Bi. Muthoka alianza akiwa mchanga mno. La kushangaza ni kuwa ushuhuda wake ndio unaompa motisha ambao ni mateso na shida alizopitia.

"Babangu alikufa Januari 1999, mamangu akafa mwaka huo huo Februari. 2000 dadangu mkuu akafa 2001 wawili wakafa, 2002 mke wa ndugu yangu akafariki, mwaka uliofuata ndugu yangu naye. Kila mwaka kwanzia mwaka wa 1999 nimekuwa nikipoteza watu wetu." Alisimulia msanii huyo.

"Wote ambao walibaki wawili wamekufa 2006 wasichana naye ndugu yangu akafa 2010 na kuharibu mambo dada zangu walikuwa wanafariki watu wawili wawili, kwa siku moja tulikuwa tunazika watu wawili wawili na hata la kutisha ni kuwa dada zangu walikuwa wanafariki pamoja na mabwana zao huku wakiwacha watoto wao. Hapo sasa nikafukuzwa katika boma lenye nilikuwa naishi kwani nilikuwa nimebeba laana ya kifo." Aliendeleza usimulizi wake ambao ulivunja mioyo ya wakenya wengi.

Baada ya kufukuzwa katika boma lile alikuwa ameolewa hapo akajitwika jukumu la kuwalea watoto wote kumi na saba ambao walibaki yatima akiwa pekee yake.

Skiza kanda ifuatayo ili upate matukio yote aliyopitia bi Muthoka yakiwemo kulala njaa pamoja na watoto kwa takriban wiki kadhaa kabla ya mungu kumnyunyuzia baraka zake.

&feature=youtu.be