AUDIO: Mbona Wanaume Wananiogopa? - Wavinya Ndeti

wavinya.
wavinya.
Mgombeaji wa kiti cha Ugavana cha kaunti ya Machakos anashangazwa na jinsi wapinzani wake haswa wanaume wana hofu kuu naye huku uchaguzi mkuu ukizidi kukaribia.

Akizungumza asubuhi ya leo katika mahojiano ya moja kwa moja na watangazaji wa Radio Jambo, Gidi na Ghost, Wavinya ambaye alikuwa mbunge wa eneo bunge la Kathiani, alifichua kuwa wapinzani wake wanajaribu chochote wawezacho ili azuiwe kugombea kiti hicho, huku akisema kuwa baadhi ya mbinu wanazotumia ni kueneza porojo na propaganda.

"Unajua, ni nini hawa wanaume wanaogopa?." Aliuliza Bi. Wavinya ambaye ni mgombeaji kwa tiketi ya chama cha WDM-K.

Mbona wanaogopa Wavinya sana hivo? Mpaka wanaweka propoganda wanafanya mambo mengi hata mmoja kama sasa huyu gavana ako hapa anasema eti mimi nimepanga kutoa vijana kutoka Kibera waje kutoa vita Machakos. Kwa nini hawa watu wanaogopa? Wanajaribu chochote wanachoweza ili nifungiwe nisiingie kwa debe lakini wao sio mwenyezi Mungu." Alijieleza.

Bi. Wavinya alikiri kuwa ana imani kuwa utendakazi wake wakti alikuwa mjumbe wa Kathiani ndio unaowapa wapinzani wake tumbo joto.

Akizungumzia mipango aliyo nayo kwa wakaazi wa kaunti ya Machakos, Wavinya alisema kuwa swala la maji ndilo atakalo tatua katika kipindi cha miaka miwili ya kwanza atakapochaguliwa.

"Yale mambo nitaangazia ni maji. Ukienda Mavoko hata Kathiani yale maji yanayotumika pale ni yale nilitengeneza nikiwa mheshima wa Kathiani. Nimewaambia watu wa Machakos kuwa nikishirikiana na wataalamu wa maji nitachimba visima vitatu kila kata ndogo." Alisema. 

Miaka ya kwanza miwili kuongea ukweli nikimuogopa Mungu hata afadhali niwache mambo mengine nitilie makini nihakikishe watu wetu wamepata maji."

Skiza mahojiano ya mheshimiwa Wavinya Ndeti.

&feature=youtu.be