Babu Owino 1

Baada ya Kuikomboa ‘Bedroom’ Babu Owino asema wanalenga ‘Sitting room’

Baada ya chama cha ODM kuwabwaga wana Jubilee katika uchaguzi mdogo wa eneobunge la Kibra, kwa sasa mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino anasema wataka kuikomboa “Sitting room” ya ODM, eneo hilo likiwa Langata.

Eneo bunge la Langata linaongozwa na Mbunge Nickson Korir ambaye aliteuliwa kutoka chama cha Jubilee.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Babu Owino aliishangalia juhudi za ODM kuwapandua wana Jubilee katika uchaguzi wa Kibra kwa kile wanakisema ni ” Bedroom yao”.

“Tumikomboa Bedroom ya Baba, hatua inayofuata ni pale siitngroom (Langata) hawa wageni wametuozea sana!” ujumbe wake ulisoma.

Kijana Ashtakiwa Na Kufanya Mtihani Wa KCSE Kortini

Ujumbe wake ulisoma Hivi ;

Mgombea wa chama cha ODM Imran Okoth aliwabwaga wagombeaji wengine 23 kwa kuzoa jumla ya kura 24, 636, alifuatwa na McDonald Mariga wa Jubilee kwa kura 11,230, Eliud Owalo wa ANC alikuwa wa tatu kwa kura 5,275, huku Khamisi Butichi wa Ford Kenya akifunga nne bora kwa kura 260.

Hata hivyo McDonald Mariga alikubali kushindwa huku akipongeza Imran Okoth.

Alisema kwamba yuko tayari kumuunga mkono Imran kuhakisha kwamba wakaazi wa Kibra wanahudmiwa ipasavyo

Kivumbi Ndani Ya “Bedroom” Huku Raila Akimlambisha Ruto Sakafu

 

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments