Baada ya kukosa wadhamini, Gor wasaini mkataba na Agro Chemicals

agro chemicals
agro chemicals
Gor Mahia wametia saini mkataba wa ushirikiano na kampuni ya Agro Chemicals.

Mkataba huo utapelekea kampuni hio kuwapa Kogalo shilingi milioni 2, wanaojitayarisha kuchuana na DC Motema Pembe katika mechi ya marudio ya Caf Confederation.

Mkataba huu utawasaidia Gor kulipa mishahara ya wachezaji kwani imekua ikikumbwa na matatizo ya fedha kwa kukosa wadhamini.

Kocha wa Bandari Bernard Mwalala anasema bado wana uwezo wa kufuzu kwa awamu ya makundi katika kipute cha mashirika bara Afrika, licha ya kunyukwa 4-2 na Horoya ya Guinea wikendi iliyopita.

Vijana hao wa Mombasa lazima wawanyuke mabingwa hao wa Guinea 2-0 ili kufuzu kwa mabao ya ugenini. Mabingwa wa KPL  Gor Mahia nao wataelekea Kinshasa Congo leo kabla ya mchuano wa marudio dhidi ya DC Motema pembe. KO’gallo walitoka sare ya  1-1 na batoto ba Congo na lazima washinde angalau moja bila ili kufuzu.

Mathare United watawaalika Posta Rangers katika raundi ya nane ya mechi ya KPL ugani Machakos leo mchana. Vijana wa mabanda hawajafungwa katika ligi hio kufikia sasa na wako katika nafasi ya 9 na alama 10.

Posta Rangers wamepoteza mechi moja tu na wako katika nafasi ya nane na alama kumi pia kwa wingi wa mabao. Rangers watazikosa huduma za kiungo Marcelus Ingotsi anayeuguza jeraha. Joackins Atudo na Cavin Odongo pia hawatacheza.

Mshambulizi wa AFC Leopards Ismaila Diarra anaripotiwa kutaka kuondoka kutoka klabuni humo kutokana na kukiukwa kwa mkataba wake.

Ingwe inasemekana kua haijawalipa wachezaji wake kwa miezi mitatu iliyopita, kwani kama vilabu vingi humu nchini inakumbwa na matatizo ya kifedha. Ni kwa sababu hii Diarra anawataka Ingwe kumwachilia aondoke. Mwenyekiti Dan Shikanda amethibitisha kua raia huyo wa Mali anataka kuondoka.