Baada ya kuolewa rasmi nataka niwe na watoto wengi! Asema Anerlisa Mungai

NA NICKSON TOSI

Anerlisa Muigai hivi maajuzi alijumuika na mtoto wa mpenziwe Ben pol ambaye alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ,kiashiria kuwa wapenzi hao mahaba yao yalikuwa yamefika kilele zaidi.

Kutokana na picha zilizokuwa zikitumwa kwenye mitandao ya kijamii, mmoja angeona labda Anerlisa anaweza kuwa mama mzazi bora baada ya kuonekana akimkumbatia mwana Ben, wote wakiwa wanaangua vicheko.

Akiwa katika mazungumzo na wanaomfuatilia katika mitandao ya kijamii, Anerlisa alidai kuwa anapania kupata watoto na mpenziwe Ben Pol baada ya wao wawili kufunga pingu za maisha .

Unapanaga lini kupata watoto na mpenzi wako Ben?.Alimuuliza shabiki

Anerlisa akamjibu hivi, Baada ya sisi kuona rasmi na Ben, hakika nataka kuwa na watoto kwa sababu napenda sana watoto mimi.

Anerlisa na Ben Pol wamekuwa pamoja tangu mwaka 2018, uhusiano wao uliwekwa wazi baada ya wapenzi hao wawili kuwahusisha wazazi wao kutoka pande zote mbili.