Baada ya madai ya mauaji, Ruto atuma ujumbe kwa wabunge wa Jubilee

unnamed
unnamed
Naibu wa Rais William Samoei Ruto sasa anawataka wajumbe wa chama tawala cha Jubilee kujiepusha na siasa za mwaka wa 2022. Akizungumza katika maeneo ya mkoa wa Mumias magharibi, kaunti ya Kakamega, Ruto amewasihi wabunge hawa ambao wanaonekana kugawanyika katika mirengo ya TangaTanga na Kieleweke wakome siasa za ukabila na mgawanyiko.

Soma hapa hadithi :

Soma hapa:

Ruto alisisitiza kuwa msingi wa chama cha Jubilee umoja na maendeleo ya taifa.

" Siasa zetu zinatakiwa ziwe za kuyabadilisha maisha ya wakenya. Hilo ndilo jukumu letu." alisema William Ruto.

Ruto alisema kuwa maendeleo ya taifa hili yanategemea sana siasa zinazoendeshwa na wanasiasa na viongozi serikalini na katika upinzani. Ruto alionekana kukasirishwa na baadhi ya wanasiasa wanaotenga wakati mwingi kwa siasa za chuki badala ya kuchapa kazi.

Soma hapa:

Ruto aliwahimiza wanasiasa wa Jubilee kuongozwa na manifesto ya chama ili pamoja waweze kuupiga vita ukabila nchini.