Matata sana!Wahubiri hawa ni wazushi ,matajiri na sarakasi zao kuhusu Neno la mungu ni tele

Afrika  imeshuhudia  aina mpya ya wahubiri ambao wamejipata katika vichwa vya habari kwa njia mbazo sio za kawaida .wengi wao ni kutoka Nigeria ,Afrika kusini na hata hapa nyumbani Kenya .Kutoka miujiuza bandia ,hadi kuwa na mali nyingi kupundukia –baadhi ya wahubiri hawa wana ushawishi mkubwa sana  kwa waumini wao na wanachosema ni sheria au hata hutumika kama neon kutoka kwa Mungu .

Vitendo  vya baadhi yao hata hivyo  vimetilia doa ukweli wao na hata hadhi zao hasa machoni pa watu .Kinachoshangaza hata hivyo ni kwamba licha ya  mkinzano wa vitendo na mahubiri yao ,bado wanaaminika sana na wafuasi wao ambao huwatetea na kuwafuta kote . Kuna baadhi ya watu hasa wanawake ambao huamini na kuogopa kila wanachoambia na wahubiri wao.Kuna visa ambavyo vinajulikana  vya watu kungoja wataoana lini au ahata kuoa nani watakapoambiwa na mhubiri wao! Hii hapa orodha ya baadhi ya wahubiri wazushi na wanaojulikana kwa sababu  moja au nyingine –nzuri au mbaya .

5.Victor Kanyari aka Bishop Mwangi

  Pastor Kanyari  anajulikana sana kwa miujiuza yake ‘feki’ na hata alijipata pabaya wakati makala maalum ya runinga yalipomuangazia akifanya utapeli wake .Pia amefahamika sana kwa wito na ombilake la sadaka ya shilingi 310. Baada ya kuvurugika kwa sifa  na jina lake .aliamua kubadilisha jina lake na sasa anafahamika kama  Bishop Mwangi . Chini ya  jina jipya na sifa tofauti siku hizo anaitisha sadaka ya shilingi 250  .wakati alipokuwa katika kilele cha utapeli wake ,alifanya miujiza yake kutumia kemikali ya  potassium permanganate,  iliyokuwa ikgeuka rangi kuwa ya zambarau  inapowekwa majini .