Baadhi ya wanamichezo walipatwa pabaya na sheria ni;
Ezekiel Kemboi
Ezekiel Kemboi ni mwanariadha shupavu wa mbio za kuruka vyiunzi lakini mwaka wa 2012 alijipata mikononi mwa polisi kwa kumshambulia mwanamke aliyefahamika kama Ann Njeri.
Kemboi aliachiliwa kwa dhamana ya shillingi 50,000, baada ya kukana madai hayo baadaye mwaka huo mwanamke huyo aliondoa mashtaka dhidi ya Kemboi na kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Frank Wanyama
Mwaka wa 2018 staa wa raga alishtakiwa kwa kumbaka msanii mmoja humu nchini na kuhukumiwa miaka 15 gerezani.
David Gikaria
Alikamatwa na maafisa wa DCI na kushtakiwa kwa makosa kumi, likiwemo unyakuzi wa ardhi ya umma katika kaunti ya Nakuru.
Alex Olaba
Alishtakiwa pamoja na Frank Wanyama kwa kumnajisi na kumbaka msanii mmoja nchini. Alihukumiwa miaka 15 gerezani.
Stephen arap Soi
Alishtakiwa mwaka wa 2016 kwa kufuja shilingi milioni 4.9 za wachezaji wakati wa michezo ya Olimpiki nchini Brazil.
Robinson Njoroge
Alifikishwa katika mahakama ya Kibera kwa madai ya wizi wa mabavu, wakati huo alikuwa wa timu ya Waithaka Pips. Alishtakiwa kwa kumuibia Alex Kimantho pikipiki na simu ya shilingi 93,000.