Baba Ampiga Na Kumjeruhi Mwanawe Kwa Kukosa Kuelewa Masomo

adhibu
adhibu
Polisi mjini Migori wakishirikiana na maafisa wa idara ya watoto ya kaunti ya Migori wanamtafuta mwanamume mmoja anayedaiwa kumpiga, mwanawe wa miaka minne kwa tuhuma za kukosa kumakinika, anapomfanyia masomo ya ziada katika mtaa wa Oruba kwenye kaunti hiyo.

Kulingana na afisa wa watoto wa eneo la Migori Peter Ogindo mwanamume huyo, George Odhiambo anatafutwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za

kumpiga na kumjeruhi mwanawe wa shule ya chekechea, kwa madai kuwa alikuwa hamakiniki alipokuwa akimfanyia mafunzo ya ziada.

Mama huyo aliongeza kuwa hatimaye babake alichukua kiboko na kumcharaza mtoto huyo wa miaka minne hadi akazirai, na kisha kutorokea

eneo lisilijulikana akidhani kuwa mtoto huyo ameaga dunia.

Mtoto huyo kwa hivi sasa kwa usaidizi wa mamake Na wasamaria wemeripoti dhuluma hiyo kwa polisi, ambako uchunguzi zaidi unafanyika

huku babake akitafutwa ili aweze kujibu mashtaka dhidi yake.