gidinagghostapril20th

Baba Michelle Akataa Kupatanishwa Na Mkewe Baada Ya Mkewe Kumfumania Na Mpango Wa Kando

Mama Michelle adai kwamba walikosana na bwanake mwaka uliopita mwezi wa tisa na alitaka kumwomba msamaha ili waweze kurudiana.

Haya yalifanyika baada ya Mama Michelle kugundua kwamba mumewe alikuwa na mpango wa kando.

“Tulikosana mwezi wa tisa.Tulikosania tu mpango wa kando. Bwanangu ndiye alikuwa na mpango wa kando na hivyo akatoka kwa nyumba na kutuacha peke yetu,” Mama Michelle alimwambia Ghost.

Mama Mitchelle alisema kwamba mumewe alikuwa akitoka kwenda kazini lakini hakuwa anarudi.

“Alitoka kwa mfano anaenda kazini jumatatu anakaa siku mbili kabla ya kurudi nyumbani. Nikimuuliza alikuwa wapi izo siku mbili ananiambia kwamba alikuwa kazini tu. Hapo nikafanya uchunguzi wangu nikagundua kwamba hakuna kazi yeye hufanya usiku, yeye hufanya mchana kisha anatoka. Nilipomuuliza alisema namuongelesha vibaya na kumtusi ndiyo maana akatoka nyumbani lakini mimi nilimtusi kwa sababu ya machungu niliokuwa nikipitia.”

Mama Michelle mwenye umri wa miaka thelathini na tano alisema kwamba wameoana kwa muda wa miaka takriban kumi na miwili na wana watoto wawili. Mumewe pia husaidia wanao lakini alitaka sana mumewe arudi nyumbani kwani walikuwa wamesemezana kupitia simu ya mkononi ijumaa iliyopita.

Baba mitchelle alipoingia hewani alidai kwamba yuko na kazi mingi hivyo basi hawawezi kuongea.

“Niko kazini na kazi ni mingi leo, msalimie mama mitchelle na watoto sina mengi,” alisema Baba Mitchelle.

Photo Credits: File

Read More:

Comments

comments