crime_scene_tape

Baba mkatili amchinja mwanawe Bungoma

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 22 kwa jina Emmanuel Sifuna Wanyonyi kutoka kijiji cha Imani kata ndogo ya Tongareni eneo bunge la Tongaren, Bungoma kasikazini, amemchinja mwanawe mvulana mwenye umri wa mwaka mmoja.

Akithibitisha kisa hiki naibu wa chifu wa eneo hilo Charles Masika amesema kuwa mwanamume huyo alitekeleza kitendo hicho hapo jana mwendo wa saa kumi na moja jioni wakati mamake mtoto huyo alipokuwa shambani akipalilia mahindi.

Masika aidha amehoji kuwa chanzo cha mauaji hayo ya kinyama hakichabaini bado huku mwanamume huyo akizuhiliwa katika kituo cha polisi cha Kabuchonge.

-Brian Ojamaa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments