Anne Waiguru

Baba saidia! Waiguru sasa ataka kuokolewa na Raila

Gavana wa Kirinyaga aliye mashakani baada ya wawakilishi wa kaunti yake kupiga kura ya kumuondoa afisini sasa anatafuta msaada wa kiongozi wa ODM Raila Odinga ili kujinasua kutoka kwa masaibu yake.

Licha ya bwana Odinga kukanusha kwamba  alikutana na Waiguru siku ya Alhamisi  wiki jana, kuna  juhudi kwa upande wa washirika wa gavana huyo kuhakikisha kwamba chama cha ODM Kinamsaidia asiondolewe mamlakani wakati hoja hiyo itakapowasilishwa katika seneti.

Odinga  mwishoni mwa wiki alitoa taarifa kukanusha kwamba alifanya mkutano na gavana Waiguru hatua ambayo sasa  huenda ikaashiria kwamba atapambana kivyake kujinasua  kwani  hatma yake sasa ipo katika mikono ya maseneta.

 

 

 

Photo Credits: Hisani

Read More:

Comments

comments